MAMILIONI WASHEREHEKEA MIAKA 70 YA UHURU WA PAKISTAN

Pakistan people gather to watch a firework display during Pakistan Independence Day celebrations in Islamabad, Pakistan, Sunday, Aug. 14, 2106. (AP Photo)
Wananchi wa Pakistan wakikurusha fataki kusherehekea sikukuu ya uhuru wa nchi yao mjini Islamabad, Pakistan, Jumapili, Agosti 14, 2106.

Mamilioni ya wananchi wa Pakistan wanasherehekea kumbukumbu ya miaka 70 ya uhuru kwa maandamano, fataki na kupandisha bendera nchini kote.

Waziri Mkuu Nawaz Sharif amezielekeza sherehe hizo kama zawadi kwa eneo la Kashmir lililogawanyika, huku Pakistan na India kila moja ikidai kuwa lote ni milki yake. Kwa uchache watu 58 wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi na vikosi vya India ndani ya mwezi mmoja.

"Ninaitoa sikukuu ya leo kama zawadi kwa uhuru wa Kashmir [inayokaliwa na India]. Ninaitoa zawadi kwa watu wale wanaokabiliana na ukandamizaji wa dola kwa ushujaa mkubwa lakini wakaendelea kuhuisha moyo wa kutaka uhuru,” Sharif alisema katika ujumbe wake wa siku ya uhuru.

Pia aliwakumbuka watu 70 waliouawa katika mlipuko wa hivi karibuni kwenye hospitai moja katika mji wa Quetta kusini magharibi mwa nchi hiyo, huku akiwakumbuka askari “waliotoa mhanga maisha yao kwa ajili ya kuulinda uhuru huu.”


Zaidi ya Wapakistani 50,000, wakiwemo askari 5,000, wameshapoteza maisha tangu nchi hiyo ilipojiunga katika kile kinachoitwa kama Vita dhidi ya Ugaidi mwaka 2002.

Ungana nasi katika WhatsApp: +255 712 566 595
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.