TETEMEKO LA ARDHI LAUA NA KUHARIBU MALI

Yesterday's Earthquake casualties receives
Majeruhi wakipata huduma ya kwanza kutoka kwa maafisa wa afya mjini Bukoba mkoani Kagera. Zaidi ya watu 100 waliripotiwa kujeruhiwa.Watu 10 wamethibitika kupoteza maisha na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa katika Wilaya ya Bukoba, Mkoani Kagera kufuatia tetemeko la ardhi lililoikumba Kanda ya Ziwa jana.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi amesema kuwa kuna uharibifu mkubwa kufuatia tukio hilo ambalo pia lilizua taharuki kwa wananchi.


Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani, ambalo ni shirika kubwa duniani linalofuatilia matukio kama hayo, lilisema kuwa tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa wa 5.7 katika Kipimo cha Richa.

Afisa Habari wa mkoa wa Mwanza, Atley Kuni alisema kuwa watu wengi waliacha shughuli zao na kukimbilia maeneo yenye usalama.


Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani lilisema kuwa kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa katika eneo la Nsuga, na eneo lililo jirani na Ziwa Victoria, huku kina cha tetemeko kikiwa ni kilometa 10.


Tetemeko hilo lilitokea kilometa 29 kaskazini mashariki mwa mji wa Kyaka, kilometa 41 kaskazini mwa Katoro, na kilometa 43 Kaskazini Magharibi mwa mji wa Bukoba.


Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo pia liliripotiwa katika mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara.

Aidha, Kuni alisema kuwa watu waliokuwa katika majengo marefu, hasa katikati ya jiji la Mwanza, walilazimika kuyakimbia wakati wa tetemeko hilo. “Taharuki na hofu iliwakumba wakazi wengi mjini na mkoa wote kwa ujumla kwa sababu wengi wao hawakuwa wakijua kinachotokea,” alisema.


Afisa wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania mkoa wa Mwanza, Augustino Nduganda alithibitisha kutoka kwa tukio hilo lakini akasema ni mapema kutoa taarifa za kina.
“Taarifa sahihi kuhusiana na tetemeko hili zitatolewa hivi karibuni,” alisema.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.