UCHAGUZI WA WABUNGE NCHINI JORDAN

People walk past electoral posters for candidates of Jordan’s parliamentary elections in the capital, Amman, September 16, 2016. (Photo by Reuters) 


Wananchi wa Jordan leo wameelekea kwenye vituo vya kupigia kura kuwachagua wabunge baada ya mabadiliko ya sheria za uchaguzi yaliyokishawishi chama cha upinzani cha Islamic Action Front (IAF)kurudi kwenye jukwaa la kisiasa baada ya kupita muongo mmoja.

Mchakato wa upigaji kura ulianza leo asubuhi na unatarajiwa kudumu kwa muda wa saa 12.

Zaidi ya wapiga kura milioni 4 wenye umri wa miaka 17 wanatarajiwa kuwachagua wabunge 130 kati ya wagombea 1,252 watakaohudumu kwa muhula wa miaka 4.

Miongoni mwa viti hivyo, viti 15 vimetengwa kwa ajili ya wanawake, 8 kwa ajili ya Wakristo na 3 kwa ajili ya wawakilisha wa Wachechenia na Circassia ambao wanaunda jamii za watu wachache nchini humo.

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi nchini humo, waangalizi wa ndani wapatao 14,000 na wengine 676 kutoka nje ya nchi wanafuatilia uchaguzi huo. Miongoni mwa waangalizi hao, waangalizi 66 ni kutoka Jumuiya ya Umoja wa Ulaya.

Hayo yanatokea wakati ambapo chama cha Islamic Action Front (IAF)--- chama cha upinzani chenye nguvu – ambacho kiligomea chaguzi mbili zilizopita, kilitangaza mwezi Juni kuwa kingeshiriki uchaguzi huo baada ya sheria ya uchaguzi kufanyiwa ya mabadiliko.


Chama cha IAF, ambalo ni tawi la kisiasa la vuguvugu la Udugu wa Kiislamu (Muslim Brotherhood), kilishiriki katika uchaguzi wa bunge wa mwaka 2007, lakini kiligomea chaguzi za mwaka 2010 na 2013 kikipinga mfumo wa uchaguzi na tuhuma za wizi wa kura.


Msemaji wa chama hicho, Murad Adayleh, ambaye pia ni miongoni mwa wagombea, amesema kuwa chama chake kitasukuma agenda ya mabadiliko ya kiuchumi na kielimu katika harakati za “kufichua sera mbovu za serikali na kuweka wazi makosa yote ya sera hizo”.

Alisema kuwa chama chake kinatarajia kushinda kuanzia robo moja mpaka theluthi moja ya viti 130 vya ubunge.

Sheria moya za uchaguzi unaviruhusu vyama kuwa na orodha kubwa, badala ya mfumo wa “kura moja” ambao uliwanufaisha wagombea wa makabila, kwa mujibu wa serikali. Walibadilisha mfumo wa “mtu mmoja, kura moja” ambao uliwekwa mwaka 1993 na kuvidhoofisha vyama vya kisiasa.

Hata hivyo, wakosoaji wanasema kuwa mabadiliko ya mfumo huo bado yanaendelea kuwanufaisha na kuwapendelea wafuasi wa kikabila wa Mfalme Abdullah II wa nchi hiyo. Wanasema kuwa bunge jipya litakuwa sawa na bunge linalomaliza muda wake, ambalo lilikosolewa na wananchi kwa kushindwa kushughulika tatizo la ukosefu wa ajira na matatizo mengine.

Mapema mwaka 2015, bunge lilipitisha mabadiliko ya kikatiba yaliyompa mfalme haki ya moja kwa moja kuwaajiri na kuwafukuza wakuu wa jeshi, wakuu wa  idara za usalama, majaji na wabunge wa bunge la seneti bila ithibati ya serikali.


Kabla ya hapo, haki pekee ya mfalme Abdullah II ilikuwa ni kumteua moja kwa moja waziri mkuu.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.