MAWIMBI YA MOTO YAITIKISA ISRAEL KWA SIKU YA NNE

 A picture taken on November 24, 2016 shows a fire raging in Haifa, northern Israel, November 24, 2016. (By AFP)

Moto wa nyika umeendelea kushika kasi kwa siku ya nne mfululizo baada ya moto mkubwa kuibuka katika mji wa Haifa, kaskazini magharibi mwa Israel na kuwalazimisha maelfu ya watu kuondoka kwenye makazi yao.

Leo Ijumaa mawimbi ya moto yalishika kasi kwenye maeneo mengi yanayokaliwa kimabavu na utawala wa Israel. Moto uliozuka mjini Haifa, ambao ndio mji ulioathiriwa zaidi, uliwalazimisha zaidi ya watu 80,000 kuyakimbia makazi yao na kutafuta sehemu yenye usalama zaidi.

Aidha, moto huo bado unaendelea kushika kasi kwenye misitu ya eneo la magharibi mwa Jerusalem, kwenye vilima vya katikati na kaskazini na maeneo ya Ukanda wa Magharibi unaokaliwa kimabavu.

Polisi wamesema kuwa usiku kucha watu waliondolewa katika kijiji cha Beit Meir jirani na Jerusalem. Pia waliripoti kuzuka kwa moto moya jirani na mji wa kusini wa Kiray Gat.

Meya wa mji wa Haifa aliwataka wakazi wenye vifaa vya kumwaga maji kusaidia kuzima moto huku maelfu ya wakazi wa mji huo wa pwani wenye mchanganyiko wa Wayahudi na Waarabu wakikimbilia kwenye makazi ya muda.

Baadaye leo asubuhi mamlaka zilisema kuwa moto ulikuwa umedhibitiwa, lakini ikatahadharishwa kuwa mambo yangeweza kubadilika kwa kuwa upepo mkali unafanya mambo yasitabirike.


Tangu kuanza kwa moto huo katika mji wa Haifa, wazima moto wa Israel wamekuwa wakijaribu kuzima maeneo 200, gazeti la Jerusalem Post limeripoti. Eneo lote la mji huo wa pwani halina watu, sambamba na eneo la Chuo Kikuu cha Haifa na magareza ya eneo hilo.

Serikali ya Tel Aviv imekuwa ikiomba msaada kutoka nje ili kukabiliana na wimbi la moto huo.

Ukosefu wa vifaa, hali ya hewa mbaya na upepo mkali vimechangia kusambaa kwa moto huo katika maeneo yote ya Israel.


Ndege ya kuzima moto ikisaidia kuzima moto mjini Haifa, Novemba 24. 2016

“Hali ya hewa imefanya iwe rahisi kwa moto huo kusambaa”, amesema Noah Wolfson, ambaye ni mtendani mkuu wa kampuni inayohusika na utabiri wa hali ya hewa ya Meteo-Tech. “Hali ya hewa itaendelea kuwa kavu, angalau mpaka Jumatatu au Jumanne.”


Hata hivyo, maafisa wa Israel wametoa lawama ya moto huo dhidi ya Waarabu au Wapalestina wakiwaita kuwa ni “magaidi”.

Tuhuma hizo zinakuja wakati utawala wa Israel ukiwa kwenye shinikizo kubwa dhidi ya shughuli haramu za ujenzi wa makazi ya walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa kimabavu.

Waziri wa elimu wa Israel, Naftali Bennett, ambaye ni mtetezi mkubwa wa unyakuzi wa ardhi za Wapalestina unaofanywa na utawala huo, amesema kwenye mtandao wa Twitter kwamba wahusika ni “wahujumu” ambao sio watiifu kwa Israel, akimaanisha kuwa wale waliowasha moto huo sio Waisrael.


Madai hayo yamekikasirisha chama cha Fatah cha Rais wa Mamlaka ya Wapalestina Mahmoud Abbas, ambacho kimesema kuwa utawala wa Tel Aviv “unatumia kisingizio cha moto huo” kutoa tuhuma mpya dhidi ya Wapalestina.

“Kinachoungua ni miti yetu na ardhi yetu ya Palestina ya zamani,” kilisema chama hicho chenye makao makuu katika eneo la Ukanda wa Magharibi.Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.