MOTO WAVAMIA BWENI LA WASICHANA NA KUUA 12 KUSINI MWA UTURUKI

 


Watu 12 wamepoteza maisha yao na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya moto kuzuka katika bweni la wasichana katika jimbo la Adana kusini mwa Uturuki.

Mfanyakazi mmoja na wanafunzi 11 wenye umri wa kati ya miaka 10 na 16 wamepoteza maisha katika moto huo, mkuu wa kikosi cha zimamoto mjini Adana amasema.

Gavana wa Adana, Mahmut DemirtaƟ amethibitisha idadi hiyo na kuongeza kuwa watu wengine 22 waliokolewa na kupelekwa hospitali. DemirtaƟ amesema kuwa wanafunzi waliojeruhiwa waliathiriwa na moshi na baadhi yao walijeruhiwa na vioo wakati wakikimbia.

Amesema kuwa moto huo ulizuka baada ya mita ya umeme katika jengo hilo kushika moto, lakini uchunguzi bado unaendelea.CHANZI: Daily Sabah
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.