BALOZI WA URUSI NCHINI UTURUKI AUAWA

Balozi wa Urusi nchini Uturuki, Andrey Karlov, akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya sanaa mjini Ankara Uturuki Desemba 9, 2016. Balozi huyo ameuawa kwa kupigwa risasi. 


Balozi wa Urusi nchini Uturuki, Andrey Karlov, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na mtu asiyejulikana wakati alipokuwa akizinduia maonesho ya sanaa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Ankara.

Mshambuliaji huyo aliuawana kikosi maalum kwenye eneo hilo la Wilaya ya Çankaya katikati mwa Ankara.

Balozi Karlov alipelekwa hospitalini baada ya kupigwa risasi mara nane ambapo watu wengine kadhaa walijeruhiwa.

Maafisa wa serikali ya Urusi wamesema kuwa shambulizi hilo lilifanywa na mtu mwenye siasa na mtazamo mkali.

Picha ikimuonesha muuaji wa Balozi wa Urusi nchini Uturuki akiwa amemsimamia baada ya kumpiga risasi balozi huyo wakati wa ufunguzi wa maonesho ya sanaa mjini Ankara Uturuki, Desemba 19, 2016. 

"Wakati balozi akitoa hotuba, mtu mmoja mrefu aliyevalia suti alianza kupiga risasi juu kisha akamlenga balozi,” amesema shuhuda mmoja. “Alisema kitu fulani kuhusu ‘Aleppo’ na ‘kisasi’.”Picha zilimuonesha mtu huyo aliyevalia suti nyeusi akiwa ameshika bastola na amesimama jirani na eneo la kutolea hotuba ambalo kuta zake zilikuwa zimetundikwa picha mbalimbali. Watu wanne akiwemo mtu aliyeonekana kuwa balozi, walikuwa wamelala sakafuni.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Urusi, Maria Zakharova, amesema katika taarifa iliyorushwa kwenye televisheni kuwa wizara yake itatoa tamko kuhusu shambulizi dhidi ya balozi huyo.


Taarifa zaidi itawajia hapa hapa....
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.