UCHAGUZI WA GAMBIA: WAPIGA KURA HUTUMIA GOLOLI KUMCHAGUA RAIS

gambia-marbles-large_transqvzuuqpflyliwib6ntmjwfsvwez_ven7c6bhu2jjnt8 


Siku ya Jumatatu tume ya uchaguzi nchini Gambia ilionesha kile ilichokielezea kuwa ni suluhisho la wizi wa kura na kwa wale wasiojua kusoma wakati wa upigaji kura. Suluhisho hilo ni upigaji kura kwa kutumia gololi.

Katika mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa nchi hiyo, Banjul, Tume Huru ya Uchaguzi (IEC) ilionesha ndoo tatu za bati zinazowakilisha wagombea watatu wanaowania kiti cha urais katika uchaguzi wa Desemba 1 katika taifa hilo dogo barani Afrika.

Wapiga kura huingia katika eneo la faragha ambalo limezibwa ambapo hudondosha gololi moja katika mojawapo kati ya ndoo tatu zilizopakwa rangi za na nembo za chama, na kengele hulia kuthibitisha kuwa kura imepigwa.

People transport ballot drums with the colours of the three parties contesting in Gambia's upcoming presidential election in Serekunda
Wafanyakazi wa tume wakisafirisha ndoo za kupigia kura zenye rangi za vyama vitatu vilivyoshiriki katika uchaguzi wa Urais nchini Gambia katika mji wa Serekunda.


“Ni kitu cha kipekee na tunajivunia,” alisema makamu rais wa IEC, Malleh Sallah, akifafanua namna Gambia ilivyobuni wazo hilo miongo sita iliyopita.

Maafisa wa tume ya uchaguzi wanasema kuwa mfumo huo unafanya pasiwepo kura zinazoharibika na kuwawezesha Wagambia wasiojua kusoma kupiga kura kwa urahisi, huku ukihakikisha kuwa kura moja pekee ndiyo inayopigwa kwa kila mtu.

Ili kuzuia sauti ya pili kusikika, ndani ya ndoo husika pamewekwa mchanga.


Katika matokeo ya kura yaliyotangazwa leo tume ya uchaguzi ilimtangaza Adama Barrow, aliyekuwa akiwakilisha muungano wa vyama vya upinzani kuwa mshindi wa kiti cha Urais huku Rais Yahya Jammeh aliyekuwa na matumaini ya kurudi madarakani kwa mara ya tano akikubali kushindwa.


Kinyang’anyiro hicho kilikuwa na wagombea watu: Yahya Jammeh aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka 22, Adama Barrow aliyewakilisha muungano wa vyama vya upinzani na Mama Kandeh wa chama cha Gambian Democratic Congress (GDC) ambaye alishika nafasi ya mwisho.

Nchi hiyo ina watu 880,000 wenye sifa za kupiga kura.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.