MLIPUKO WA BOMU WAUA 33 MJINI BAGHDAD
Kwa uchache watu 33 wamepoteza maisha na wengine 48 kujeruhiwa katika shambulizi la bomu lililotegwa kwenye gari katika kitongoji chenye shughuli nyingi cha Sadr mjini Baghdad nchini Iraq, duru za kipolisi na hospitali zimesema.

Mpaka sasa hakuna kundi lililodai kuhusika lakini kundi la Daesh (Dola la Kiislamu katika Iraq na Sham) mara kwa mara limekuwa likiyalenga maeneo ya raia katika mji huyo wenye ulinzi mkali.

Mapema siku ya Jumamosi mashambulizi matatu ya bomu yaliwaua watu 29 katika mji huo. Shambulizi lingine la Jumapili liliwaua polisi saba.

Vikosi vya serikali kwa sasa vinapambana kuliondoa kundi la Daesh katika mji wa kaskazini wa Mosul, ambao ndio ngome kuu ya mwisho ya kundi hilo katika nchi hiyo, lakini kumekuwa na upinzani mkali.

Tangu operesheni hiyo ilipoanza Oktoba 17, vikosi maalum vimeichukua robo ya mji huo katika operesheni kubwa kabisa ya ardhini kutokea nchini humo tangu Marekani ilipofanya uvamizi mwaka 2003 na kumuondosha kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, marehemu Saddam Hussein.

Waziri Mkuu Haider al-Abadi amesema kuwa mpaka Aprili kundi hilo litaondoshwa kikamilifu katika maeneo yote ya nchi hiyo.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.