RAFSANJANI AFARIKI DUNIA

 Chairman of the Expediency Council Ayatollah Akbar Hashemi Rafsanjani passes away due to heart disease.

Aliyewahi kuwa Rais wa Iran Hashemi Rafsanjani amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82 kutokana na mshituko wa moyo.

Rafsanjani alipelekwa hospitali moja kaskazini mwa mji wa Tehran baada ya kusumbuliwa na tatizo hilo.

Mwanasiasa huyo mashuhuri aliyezaliwa Agosti 25, 1934, alikuwa rais wa nne wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliyehudumu kuanzia mwaka 1989 mpaka 1997.

Rafsanjani alikuwa mkuu wa Baraza la Wataalamu kuanzia mwaka 2007 mpaka 2011. Mwanadini huyo alichaguliwa kuwa spika wa bunge la Iran mwaka 1980 nafasi aliyoendelea kuishikilia mpaka mwaka 1989. Aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kuanisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu nchini humo mwaka  1989.

Ayatollah Hashemi Rafsanjani alikuwa miongoni mwa wasaidizi waandamizi wa kiongozi wa zamani wa taifa hilo, Hayati Imam Khomeini.

Alikuwa na mchango mkubwa wakati wa mapambano ya kupinga utawala wa mfalme Shah kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na baadaye katika hatua mbalimbali za kuasisiwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Wakati wa vita vya Iraq na Iran vilivyodumu kwa muda wa miaka 8, Rafsanjani alichukua nafasi ya kaimu amiri jeshi mkuu wa vikosi vya majeshi ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran (IRNA), mazishi ya Hashemi Rafsanjani yatafanyika siku ya Jumanne mjini Tehran.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.