SHAMBULIZI LA KIGAIDI LAUA WATU 39 NA KUJERUHI 69 MJINI ISTANBUL

Terror attack on Istanbul nightclub leaves 39 dead, 69 wounded


Mshambuliaji aliyevalia vazi la Krismasi maarufu kama Santa Claus alifyatua risasi kwenye ukumbi mmoja wa usiku mjini Istanbul wakati wa sherehe za kuukaribisha Mwaka Mpya.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki, Süleyman Soylu, shambulizi hilo limewaua watu 39 na kuwajeruhi wengine 69.

Soylu amesema kuwa watu 16 miongoni mwa waliouawa walitambuliwa kuwa raia wa kigeni, huku 5 wakiwa raia wa Uturuki. Juhudi zinaendelea kuwatambua miili ya watu wengine 18. Aidha, waziri huyo ameeleza kuwa majeruhi 69 wako hospitalini wakipatiwa matibabu.

“Majeruhi 4 wako katika hali mbaya. Mmoja amejeruhiwa vibaya sana,” amesema Soylu.

Afisa mmoja wa serikali ni miongoni mwa waliouawa katika shambulizi hilo lililoulenga ukumbi wa Reina unaopatikana katika kitongoji cha Ortaköy mjini Istanbul. Duru zinasema kuna uwezekano kwamba kulikuwa na washambuliaji zaidi ya mmoja waliohusika katika shambulizi hilo. Wakati wa shambulizi hilo zaidi ya watu 500 walikuwa ndani ya ukumbi huo.

Mshambuliaji alianza kuwafyatulia risasi polisi waliokuwa nje ya ukumbi kabla ya kuingia na kuwafyatulia watu waliokuwa ndani. Baadhi ya wateja walijirusha kwenye maji katika mkondo wa Bosporus ili kujinusuru na shambulizi hilo.

Polisi wameanzisha msako mkubwa kumsaka mshambuliaji huyo ambaye alifanikiwa kukimbia baada ya kufanya tukio hilo.

Hatua za kiusalama zimeimarishwa katika miji mikubwa nchini Uturuki huku polisi wakiweka vizuizi kwenye maeneo muhimu ya kuelekea katika miji ya Istanbul na Ankara.


Miji ya Ankara na Istanbul ililengwa na mshambulizi kadhaa kwa mwaka 2016 yaliyotekelezwa na wapiganaji wa makundi ya Daesh na PKK na kuuawa zaidi ya watu 180.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.