WABUNGE WA GAMBIA WAONGEZA MUDA WA JAMMEH KUBAKI MADARAKANI
Bunge la Gambia limepitisha azimio linalomruhusu Rais Yahya Jammeh kubaki madarakani kwa miezi mitatu zaidi, kuanzia leo, kwa mujibu wa televisheni ya serikali.

Jammeh, ambaye ameitawala Gambia kwa miaka 22, mwanzo alikubali kushindwa na Adama Barrow katika uchaguzi w mwezi Desemba, lakini baadaye aliyapinga matokeo kwa madai kuwa yalikuwa na dosari na kupeleka madai yake kwenye Mahakama ya Juu ya nchi hiyo.

Barrow anatarajiwa kuapisha Alhamisi.


Mapema Jumanne Rais Jammeh alitangaza hali ya hatari, siku chache kabla ya muda wa kung’atuka madarakani kuwadia, huku mashirika na makapuni ya utalii kutoka Uingereza na Ujerumani yakifanya harakati za kuwaondosha maelfu ya watalii kutoka nchini humo.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.