WAZIRI WA SERIKALI YA BURUNDI AUAWA

Emmanuel Niyonkuru, 54, the country's water,
Emmanuel Niyonkuru, 54, waziri wa maji, mazingira na mipango, aliuawa usiku wa manane. Waziri wa mazingira nchini Burundi ameuawa usiku wa Jumapili, polisi wamesema. Mauaji hayo ni ya kwanza ya aina yake tangu nchi hiyo ilipotumbukia katika ghasia za kisiasa mwaka 2015.

Emmanuel Niyonkuru, mwenye umri wa miaka 54, ambaye alikuwa waziri wa maji, mazingira na mipango aliuawa usiku wa manane, kwa mujibu wa ujumbe uliotumwa kwenye mtandano wa Twitter na msemaji wa polisi Pierre Nkurikiye.

Mauaji hayo ambayo ni ya kwanza dhidi ya waziri anayehudumu katika serikali tangu Burundi ilipotumbukia katika mzozo wa kisiasa kufuatia uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu mwaka 2015, yamekuja baada ya miezi kadhaa ya utulivu.

"Waziri wa maji na mazingira ameuawa na mhalifu mwenye silaha wakati akielekea nyumbani kwake Rohero, kwenye saa 6:45 usiku," Nkurikiye aliandika zikiwa zimepita saa nne baada ya tukio hilo.

Aliongeza kuwa mwanamke mmoja amekamatwa kufuatia “mauaji” hayo.

Aidha, kwenye mtandao wa Twitter, Rais Nkurunziza alitoa salamu za rambirambi kwa “familia na Warundi wote" akiapa kuwa uhalifu huo utachukuliwa hatua.


Kwa uchache watu 500 wameuawa na wengine 300,000 wameikimbia nchi hiyo tangu ghasia zilipozuka mwezi Aprili mwaka 2015.

CHANZO: Daily Monitor
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.