RAIS MACRON: UFARANSA ILIKOSEA KUSHIRIKI VITA DHIDI YA LIBYA

Image may contain: 1 person, suit 


Rais mpya wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amekiri kuwa “uvamizi” uliofanywa na majeshi ya kigeni dhidi ya utawala wa Kanali Muammar Gadhafi mwaka 2011 lilikuwa kosa huku akisema kuwa Ufaransa ilifanya kosa kushiriki vita hiyo.

Rais Macron amesema katika taarifa moja kuwa “uingiliaji kati wa nchi za Magharibi lilikuwa kosa”.

Itakumbukwa kuwa mwaka 2011, Ufaransa chini ya rais Nicolas Sarkozy, ilikuwa kinara wa kuchochea uvamizi dhidi ya Libya na kulifanya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kutoruhusu ndege za Libya kuruka.

Ndege za Umoja wa Kujihami wa nchi za Mgharibi, NATO, ikiwemo Ufaransa, ziliishambulia nchi hiyo ya Afrika Kaskazini na kuwatuma askari kwa lengo la kuwasaidia waasi kumuondosha madarakati Kanali Muammar Ghaddafi.

Ghaddafi aliuawa lakini mambo yakawa mabaya zaidi.

Nchi za Magharibi ziliondoka na kuliacha jeshi la nchi hiyo likiwa taabani. Ombwe la usalama na kuzaa kwa silaha vilichochea kuibuka kwa makundi ya wanamgambo yaliopambana kutaka madaraka na mali.

Hali hii ya ukosefu wa uthabiti ilitengeneza mazingira salama kwa makundi ya kigaidi. Makundi hayo yalitumia fursa ya mapigano na mzozo wa ndani kati ya mirengo ya kisiasa na wanamgambo.


Kutokana na kutawaliwa na jangwa kwa sehemu kubwa na kuwa karibu na Ulaya kwa njia ya bahari, Libya imekuwa kivutio kwa walanguzi na safari za wahamiaji. Mambo yote hayo yamekuwa tishio dhidi ya uhai wa dola ya Libya.

Urejeshaji wa amani na uthabiti imekuwa ndoto.

Macron amekiita kitendo cha uvamizi wa mataifa ya Magharibi nchini humo kuwa ni kosa. Lakini sio kosa la kwanza; kwani kosa kama hilo lilifanyika Iraq baada ya kuanguka kwa Saddam Hussein.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.