APIGWA RISASI HADHARANI KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA MITATU


Wanaharakati wamerusha video inayoonesha tukio la adhabu ya kifo kwa kupigwa risasi katika mji mkuu wa Yemeni, Sanaa, dhidi ya mtu aliyetuhumiwa kumbaka mtoto mdogo na kumuua.

Katika video hiyo anaonekana mtuhumiwa akiwa amefungwa mikono yake kwa nyuma na amelazwa kifudifudi kisha akaonekana mtu mmoja aliyevalia sare za jeshi akiwa na bunduki na kumpiga risasi kichwani mbele ya umati wa watu ambao walipaza sauti zao na kushangilia.

Inaelezwa kuwa uhalifu huo wa kumbaka na kumuua mtoto aitwaye Rana Yahya Al-Matry mwenye umri wa miaka mitatu uliotokea siku moja kabla ya sikukuu ya Eid Al-Fitr, ulisababisha mshituko mkubwa nchini humo kiasi cha kuufanya umma ulaani na kutaka mhusika kuchukuliwa hatua kali. Mhalifu huyo aitwaye Mohamed Mujahid al-Maghriby mwenye umri wa miaka arobaini alikamatwa, akakiri kumteka na kumbaka Rana akatoa maelezo kamili ya namna alivyotekeleza uhalifu huo.

Tunaomba radhi kwa kutorusha video hiyo kutokana na picha zake.


Mtoto Rana na mbakaji wake


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.