GEORGE WEAH KUWANIA TENA URAIS

 George WeahGeorge WeahGeorge WeahImage result for george weah for president


Baada ya muongo mmoja akiwa madarakani, rais wa kwanza mwanamke kuchaguliwa kuwa r’ais barani Afrika, Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, anatarajiwa kung’atuka madarakani baada ya uchaguzi wa urais utakaofanyika mwezi Oktoba.

Kuna jumla ya wagombea 20 wanaowania kumrithi mwanamama huyo, lakini hakuna mgombea anayeonekana kuwa kinara. Hata hivyo, mcheza soka maarufu wa zamani George Weah, aliyeshindwa na Bibi Ellen Srleaf katika uchaguzi wa mwaka 2005 anatarajiwa kutupa karata yake tena.

Mbali na Weah, mbabe wa vita wa zamani Prince Johnson naye anatarajia kugombea.

Image result for Ellen Johnson Sirleaf
Rais wa sasa wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf


Vyombo vya habari vinasema kuwa katika orodha hiyo kuna mwanamke mmoja tu, naye ni MacDella Cooper, aliyewahi kuwa manamitindo, lakini kwa sasa anajishughulisha na utoaji wa huduma za kiutu.


Hii itakuwa mara ya pili kwa George Weah kuwania kiti hicho.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.