MISIKITI ZAIDI KUFUNGWA NCHINI UFARANSA

French President Emmanuel Macron delivers a speech during a special congress gathering both houses of the parliament at the Versailles Palace, near Paris, France, July 3, 2017. (Photo by Reuters)
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitoa hotuba wakati wa mkutano maalum ulioyakutanisha mabunge mawili ya nchi hiyo kwenye Kasri la Versailles, jirani na Paris, Ufaransa, Julai 3, 2017.

Bunge la Ufaransa limepiga kura kuongeza muda wa hali ya hatari nchini humo kwa kipindi cha miezi sita zaidi, huku serikali ikitangaza kuwa itafunga misikiti mitatu zaidi kama sehemu ya hatua hiyo.

Mapema Alhamisi, wabunge nchini humo walipitisha azimio hilo kwa kura 137 dhidi ya 13. Hali hiyo itaendelea mpaka mwezi Novemba. Hii ni mara ya sita kuongozwa kwa muda wa hali ya dharura.

Hali ya dharura huvipa vikosi vya usalama uhuru zaidi wa kufanya uvamizi na upelelezi. Pia huzipa mamlaka uwezo wa kuzuia safari za watu na magari katika nyakati na maeneo maalum.

Misikiti itakayoonekana kufumbia macho ugaidi itafungwa chini ya hali hiyo ya hatari.

“Leo kuna misikiti mitatu tunayotaka kuifunga,” Waziri wa Mambo ya Ndani Gerard Collomb alisema na kuongeza: “Tangu kuanza kwa hali ya hatari tumeifunga misikiti 16.”

Ni mara ya kwanza hali ya hatari kuongezewa muda chini ya utawala wa Rais Emmanuel Macron, ambaye hapo mwanzo alikuwa ameahidi kuiondosha lakini pia chini ya muswada mpya baadhi ya hatua zimegeuzwa kuwa sheria za kudumu.

Aidha, Collomb alieleza kuwa kuna sababu njema ya kuongeza muda wa hali ya hatari.

“Ni hakika kwamba tunahitaji kuongeza muda wa hali ya hatari. Kwa nini? Kwa sababu tangu kuanza kwa mwaka huu, tumefanikiwa kuzuia mashambulizi saba ambayo yangewaathiri watu wengi,” alisema Collomb.


Miaka kadhaa nyuma Ufaransa iliwahi kukumbwa na mashambulizi ya kigaidi ya mara kwa mara ambayo yaliwaua watu wengi kuliko nchi nyingine yoyote ya Ulaya. Mfululizo wa mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea Novemba mwaka 2015 yaliua watu 130 na kuifanya serikali ya Rais wa wakati huo Francois Hollande kutangaza hali ya hatari kwa mara ya kwanza.

Hali ya hatari na muswada huo wa sheria uliowasilishwa na serikali ya Rais Macron vimekoselewa na mashirika ya haki za binadamu ambayo yanasema kuwa zinaminya uhuru wa kiraia.Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.