MZOZO WA GHUBA: QATAR KUADHIBIWA ZAIDI

Egyptian Foreign Minister Sameh Shoukry (R) shakes hands with his Saudi counterpart Adel al-Jubeir (R) as UAE Minister of Foreign Affairs and International Cooperation Abdullah bin Zayed Al Nahyan stands by, during a joint press conference after their meeting in the Egyptian capital Cairo, July 5, 2017. (Photo by AFP)
Waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry (kulia) akisalimiana na mwenzake wa Saudi Arabia Adel al-Jubeir (kushoto). Wakati wa mkutano wa pamoja kwa vyombo vya habari baada ya kikao chao kilichofanyika mjini Cairo nchini Misri Julai 5, 2017. Pembeni ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa wa Umoja wa Falme za Kiarabu Abdullah bin Zayed Al Nahyan.

Nchi za Saudi Arabia, Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain zimesema kuwa ziko tayari kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya Qatar kufuatia hatua ya Doha kuyakataa masharti yao ya kukomesha mzozo wa kidiplomasia unaoendelea kati ya Qatar na mataifa hayo.

Katika taarifa yao iliyotolewa mapema leo, mataifa hayo manne yanasema kuwa kitendo cha Qatar kukataa mapendekezo yao kinaonesha namna nchi hiyo inavyounga mkono ugaidi na kuendeleza juhudi za kuvuruga usalama na amani katika eneo hilo.

Mataifa hayo unaituhumu Qatar kuwa haijali usalama na inaenda kinyume na maslahi ya wananchi wa ukanda huo.

Aidha, walimshukuru Amiri wa Kuwaiti Sheikh Sabah al-Ahmad al-Jaber al-Sabah kwa juhudi zake za usuluhishi na kuikosoa vikali Qatar kwamba inamuangusha kwa kutaka kuurejesha mzozo huo katika hatua ya mwanzo kabisa.

Mnamo Juni 5, mataifa hayo yalikata rasmi uhusiano wake na Qatar baada ya kuituhumu kuwa inaunga mkono “ugaidi” na kuvuruga amani ya Mashariki ya Kati, tuhuma ambazo Qatar inasema hazina uhalali wowote na kwamba zinatokana na madai ya urongo.

Katika hatua ya wazi ya kutaka uungaji mkono Kutoka Marekani na Israel, mataifa hayo yamesitisha safari zote za ardhini, angani na baharini kwenda na kutoka Qatar, kuwafukuza wanadiplomasia wake na kuwaamuru raia wa Qatar kuondoka katika nchi hizo.

Saudi Arabia ilifunga moja kwa moja mpaka wake wa ardhini na Qatar ili kusitisha usafirishaji wa chakula nchini humo. Hatua hiyo iliwafanya viongozi wa  Qatar kuzigeukia nchi za Iran na Uturuki kuziba ombwe hilo.

Kukifunga kituo cha utangazaji cha Al Jazeera kilichopo mjini Doha, kukata uhusiano wa kidiplomasia na Iran, kufunga kambi ya kijeshi ya Uturuki nchini Qatar na kulipa kiwango fulani pesa kama fidia ni miongoni mwa masharti ambayo mataifa hayo yaliipatia Qatar ili kumaliza mgogoro huo.

Doha inasema kuwa vikwazo ilivyowekewa ni “hujuma ya wazi” na masharti yaliyotolewa ili kuviondosha hayana “uhalisia”.

Mnamo siku ya Jumatano, waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani, alisema kuwa masharti ya mataifa hayo yanamaanisha Qatar kusalimisha mamlaka na uhuru wake.

Pia aliondoa uwezekano wa maridhiano ya haraka na kusema kuwa nchi yake iko tayari na imejiandaa kikamilifu iwapo mzozo huo utaendelea zaidi.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.