TANZIA: KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI, HASSAN SHEBUGE AFARIKI DUNIA

 


Katibu Mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi anasikitika kutangaza kifo cha Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge (pichani) kilichotokea Julai 06, 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbini Jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu. Kabla ya kufikwa na Mauti, inaelezwa kuwa Marehemu Shebuge aliugua ghafla akiwa nyumbani kwake, Mbagala Majimatitu mnamo Julai 03, 2017 na kukimbizwa katika Hospitali ya Rangi tatu ili kupatiwa huduma ya dharura na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi hadi hapo mauti yalipomfika.

Kwa mujibu wa taarifa ya kitaalamu iliyotolewa na madaktari, inaelezwa kuwa Maremu Shebuge alipatwa na shinikizo la damu ambalo limepeleka kupoteza  maisha.

Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu, aiweke roho ya Marehemu Hassan Rashid Shebuge mahala pema Peponi, Amin.

Msiba upo nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu.


IFUATAYO NI RATIBA NZIMA YA MSIBACHANZO: http://richard-mwaikenda.blogspot.com/2017/07/tanzia-karani-wa-baraza-la-mawaziri.htmlShare on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.