WLADIMIR KLITSCHKO ATANGAZA KUSTAAFU MASUMBWI

Ukranian WBA, WBO, IBO and IBF heavyweight world champion boxer Wladimir Klitschko, poses with his belts at the Esprit Arena in Duesseldorf, Germany, 21 July 2015. (EPA Photo)

Bingwa wa uzani wa juu wa WBA, WBO, IBO na IBF kutoka Ukraine Wladimir Klitschko, akiwa amepozi na mikanda yake kwenye medani ya Esprit Arena mjini  Duesseldorf, Ujerumani, 21 Julai 2015.Bingwa wa zamani wa uzani wa juu duniani, Wladimir Klitschko, ametangaza rasmi kustaafu mchezo wa masumbwi.

Mwanamasumbwi huyo raia wa Ukraine mwenye umri wa miaka 41 aliyeanza masumbwi ya kulipwa mwaka 1996 baada ya kushinda medali ya dhahabu katika michezo ya Olympic mjini Atlanta, alitawala medani ya uzani wa juu kwa muongo mmoja lakini akapoteza pambano lake na Anthony Joshua raia wa Uingereza mwezi Aprili baada ya kupigwa katika raundi ya 11.

"Kama mwanamasumbwi mzoefu na mkomavu, nimefanikisha kila kitu nilichokitamani, na sasa ninataka kuanza maisha yangu mengine baada ya michezo," Klitschko alisema katika taarifa iliyotolewa na menejimenti yake.

Alisema kuwa kwa wiki kadhaa alitafakari kabla ya kufanya uamuzi wa kuhakikisha kuwa ameusahau mchezo dhidi ya Joshua kwenye uwanja wa Wembley.

"Sikudhani kuwa ningekuwa na safari ndefu na yenye mafanikio katika mchezo kwa kiasi hicho, ninawashukuru nyote kutoka katika kina cha moyo wangu," aliwaambia mashabiki wake.

Klitscko,aliyefahamika kwa mashabiki kama 'Dr. Steelhammer,' anatundika daruga kama mmoja wa wanamasumbwi mahiri wa zama zote baada ya kutawa ubingwa wa uzani wa juu kwa muda wa miaka tisa na nusu.


Bingwa huyo alishinda mikanda kutoka vyama vya masumbwi vya WBA, WBO, IBF na IBO. Kuanzia mwaka 2008 mpaka 2012 ndugu wa Klitschko, Vitali akiwa bingwa wa WBC, walitawala ubingwa wa dunia kwa wakati mmoja na kushikilia mikanda yote muhimu ya uzani wa juu duniani.

Safari ya Wladimir Klitschko ilishuhudia akishinda mara 64 katika michezo 69, kati ya hiyo, michezo 54 alinda kwa knockouts. Alishiriki katika michezo 29 ya ubingwa wa dunia, ambayo ni rekodi ya kipekee katika masumbwi ya uzani wa juu.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.