TUNDU LISSU APIGWA RISASI DODOMA

Tundu Lissu


MBUNGE wa Singida Mashariki (Chadema) na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Tundu Lissu, amepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya.

Taarifa kutoka Dodoma zinasema, Lissu amepigwa risasi kadhaa mwilini, ikiwamo tumboni, mchana huu wakati akiingia nyumbani kwake Area D, kutokea ofisi za Bunge.

Lissu, mmoja wa wanaharakati anayepinga kwa nguvu zote utawala wa sasa kwa kuita, “utawala wa kidikteta.”

CHANZO: Mwanahalisi Online


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.