REAL MADRID WAILAZA GREMIO NA KUTWAA KOMBE LA KLABU BINGWA YA DUNIA

 Football: Real Madrid defeat Gremio, win Club World Cup


Wababe wa soka nchini Hispania, Real Madrid, wametwaa kombe la Klabu Bingwa ya Dunia baada ya kuishinda klabu ya Gremio ya nchini Brazal kwa 1-0 Jumamosi jioni mjini Abu Dhabi.

Mechi hiyo iliyosakatwa katika dimba la Zayed Sports City Stadium ilishuhudia Real Madrid ikifunga goli lake baada ya dakika ya 57 kupitia kwa nyota wake machache Cristiano Ronaldo aliyefunga kwa mpira wa adhabu.

Real Madrid walimilika mpira kwa asilimia 66 katika nusu ya kwanza ya mchezo, lakini walifanikiwa kupata goli hilo katika nusu ya pili.

Gremio walishindwa kurudisha goli hilo na kuwafanya Madrid kutwaa taji hilo kwa mara ya tatu ndani ya miaka minne na hivyo kuwa sawa na Barcelona ambao nao pia wametwaa taji hilo mara tatu.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.