MOTO WAUA 10 KATIKA KIWANDA CHA VIATU NCHINI RUSSIA

A fire burns at a construction supplies market on the outskirts of Moscow on October 8, 2017. (Photo by AFP)
Moto ukiunguza soko la vifaa vya ujenzi katika viunga vya mji wa  Moscow Oktoba 8, 2017.Kwa uchache watu 10 wamepoteza maisha baada ya moto kuunguza kiwanda cha viatu nchini Russia, huku vibarua saba wa Kichina wakiwa miongoni mwa waliofariki, maafisa wamesema.

Moto huo kwenye kiwanda kidogo katika kijiji cha Chernorechenskiy, kiasi cha kilometa 50 (maili 30) kusini mwa mji wa Novosibirsk, ulilipuka takribani saa 3 asubuhi kwa majira ya eneo hilo, vyombo vya habari vimeripoti.

Moshi mweusi uliosababishwa na kuungua kwa vifaa ulionekana kuzunguka kiwanda hicho ambacho kilikuwa na wafanyakazi 30.

"Watu wa 10 wamekufa kutokana na moto huo ambao chanzo chake kimebainishwa. Kwa mujibu wa taarifa za awali, hakuna raia wa Russia miongoni mwa waliofariki dunia," afisa wa serikali katika eneo hilo ameliambia shirika la habari la TASS.

Ubalozi mdogo wa Gina katika mji wa Ekaterinburg umesema kuwa raia saba wa Kichina wamepoteza maisha na mmoja kujeruhiwa.

Taarifa nyingine zinasema kuwa raia wa Kyrgyzstan au Tajikistan ni miongoni mwa waliopoteza maisha.

Mamilioni ya vibarua kutoka mataifa ya iliyokuwa Muungano wa Kisovieti katika eneo la Asia ya Kati huingia nchini Russia kila mwaka kufanya kazi zinazowaingizia kipato kikubwa kutokana na ukosefu wa ajira katika mataifa yao.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.