NAIBU BALOZI WA UGANDA ATIMULIWA MAREKANI KWA KUMPIGA MKE

Bwana  Dickson OgwangNaibu Balozi wa Uganda nchini Marekani ametimuliwa na Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya nchi hiyo kwa kudaiwa kumpiga mkewe.

Waziri wa nchi anayehusika na Mashauri ya Kigeni wa Uganda, Bwana Okello Oryem, amethibitisha taarifa kuwa bwana Dickson Ogwang alitakiwa mara moja kufungasha virago vyake na kurudi nchini mwake.

“Atakapofika, tutamkalisha chini yeye na mkewe ili jambo kama hilo lisitokee tena,” alisema Oryem.

Mtandao wa Daily Monitor wa nchini humo, uliripoti kwamba Bwana Ogwang aliandaa karamu kwenye makazi yake na kuwaalika wageni mbalimbali akiwemo mwanamke mmoja ambaye alikuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

Mtandao huo unasema kuwa mke wa Ogwang alielezea wasiwasi wake kuhusu mwanamke huyo baada ya wageni kuondoka, akaambulia kipigo. Pua ya mke wa Ogwang ilijeruhiwa katika tukio hilo.

Alipotoa taarifa ya tukio hilo polisi likaibuka kuwa suala kubwa la kidiplomasia baada ya mamlaka mjini Washington kutaka bwana huyo afunguliwe mashitaka.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.