WANAUME WATATU WALAZWA KWA KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME

 No automatic alt text available.


Wanaume watatu nchini Zambia wamelazwa hospitali  baada ya kunywa dawa za asili zinazodaiwa kuongeza nguvu za kiume.

 Kiongozi wa mkoa, Chanda Kasolo, amesema kuwa  mara baada ya kunywa dawa hizo, walianza kutapika kitu ambacho kilisababishwa na mchanganyiko wa chakula, pombe na dawa hizo za asili, aliiambia Bbc

''Baada ya majibu ya vipimo kupatikana , inaonekana kuwa mchanganyiko wa pombe, vyakula na dawa hiyo, ulisababisha mchafuko wa mfumo wa chakula na hivyo ikahusishwa na kipindupindu lakini baada ya kuwauliza maswali, baadaye walikiri kuwa walikunywa dawa ya kuongeza nguvu katika tendo la ndoa''

Wagonjwa hao bado wapo katika kituo hiko cha kipindupindu na wanaendelea vizuri na matibabu, aliongeza bwana Kasolo.Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.