SYRIA YAIDONDOSHA NDEGE YA KIVITA YA ISRAEL

Israeli F-16 fighter jet shot down amid Syrian anti-air fire, pilots safe - IDF
PICHA YA MAKTABA: Ndege ya kivita ya Israel aina ya F-16 


Jeshi la Syria limeilenga na kuitungua ndege moja ya jeshi la Israel aina ya F-16 ambayo ilifanya shambulizi ndani ya ardhi ya Syria, huku marubani wawili wakipona.

Jeshi la Israel limesema kuwa lilifanya mashambulizi ndani ya Syria baada ya ndege isiyo na rubani (drone) kuingia katika anga yake ikitokea Syria na kuitupia lawama Iran kwa tukio hilo.

Msemaji wa jeshi la Israel, Jonathan Conricus, amethibitisha kuwa ndege hiyo ya kivita iliangukia katika eneo la kaskazini mwa Israel, na kwamba marubani wawili wamepelekwa hospitali.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.